Ukiuwa Chatu utapata Milioni 75

Katika kipindi cha muongo mmoja tangu Florida ilipoanzisha shindano la kwanza la kuwaua chatu wa Burma, maelfu ya watu kutoka kote Marekani na duniani wameweka matumaini yao ya kuua nyoka hao kadiri wawezavyo.\

Jake Waleri, 22, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ohio ana mpango wa kuwinda chatu wakati wa mapumziko yake ya kiangazi. Alizaliwa Naples, Florida, anasema analijua swala la chatu wa Burmese.

Alivutiwa na uwindaji wa chatu baada ya kutazama wawindaji kwenye televisheni, na akaanza uwindaji miaka miwili iliyopita. Mwaka jana, aliingia Florida Python Challenge – shindano la kila mwaka la uwindaji chatu ambalo mamia ya washiriki kila mwaka kutoka nchi mbalimbali kama Canada, Ubelgiji na Latvia.

Watu huvutiwa na matarajio ya umaarufu na utajiri,kwa kushiriki shindano hilo lnalo jumuisha hadi dola za kimarekani 30,000 kama zawadi ambazo ni sawa na 75,324,687.06

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *