Viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamekutana na uongozi wa Jeshi la Magereza na kufahamishwa kuwa Mwenyekiti wao Tundu Lissu amehamishiwa katika Gereza la Ukonga.
Taarifa iliyotolewa hii leo Aprili 19, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi (CHADEMA), Brenda Rupia imeeleza kuwa familia, Wanachama wa CHADEMA na Watanzania wote waliokuwa na
wasiwasi kuhusu mahali alipo Lissu, sasa wanaweza kumtembelea kwa kufuata taratibu za kawaida katika Gereza hilo.

“Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara, Mheshimiwa John Heche, anatarajiwa kufika Gereza la Ukonga leo kwa ajili ya kumwona Mheshimiwa Tundu Lissu na kuzungumza naye kuhusu hali yake,” ilieleza taarifa hiyo.