Tayari watu watano wameomba kufanyiwa upasuaji Mloganzila

Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohammed Janabi amesema watu watano wamejitokeza kujisajili kupata huduma ya kurekebisha maumbo huku akisema zoezi hilo linalenga matibabu.

Prof Janabi amesema hadi sasa ni mgonjwa mmoja ameomba kufanyiwa huduma hiyo kwa ajili ya urembo ambapo awamu hii watafanya kwa watu 6 hadi 10.


Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Muhimbili-Mloganzila Dk Erick Muhumba Amesema kuwa wanafanya upasuaji wa aina mbili ambao wa kwanza ni upasuaji wa kupunguza uzito na upasuaji rekebishi.


Ameainisha kuwa gharama za upasuji zinatofautiana kuanzia Sh milioni 150 hadi Sh milioni 225 ambapo inategemea na mtu na aina ya upasuaji na kadiri wanavyotofautiana na gharama zinatofautiana hata kama upasuaji ni mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *