Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Tanzania yajidhatiti kuboresha sekta ya elimu

Makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango amesema Tanzania imejidhatiti kuboresha sekta ya elimu, ili kuandaa Rasilimali Watu ya kutosha kuiliendeleza Bara la Afrika.

Dkt. Mpango ametoa kauli hiyo mkoani Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, wenye lengo la kuongeza ujuzi, kuimarisha afya na elimu ya Waafrika.

Amesema Tanzania hivi sasa inapitia upya sera na sheria ya elimu, hatua itakayowezesha pia kuwaandaa wahitimu kuwa watengenezaji wazuri wa fursa mbalimbali Afrika.

Amesisitiza kuwa hayo yanawezekana kwa kuzingatia nguvukazi iliyopo nchini, kufuatia kuongezeka kwa wastani wa umri wa kuishi wa Mtanzania kutoka miaka 60 hadi kufikia miaka 66 mwaka 2022.

Aidha, kwenye masuala ya afya Makamu wa Rais amesema Tanzania imefanikiwa kupunguza tatizo la utapiamlo kutoka asilimia 34 hadi asilimia 30 iliyokuwepo mwaka 2015.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *