Yanga yapewa wadjibouti, Simba kuanzia raundi ya pili

Droo ya mechi za raundi ya kwanza (First Round) na za raundi ya pili (Second Round) ya ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho Afrika, imepangwa leo Julai 25, 2023 makao makuu ya shirikisho la soka Afrika (CAF) jijini Cairo nchini Misri, ambapo ratiba ya timu zinazoshiriki ligi ya mabingwa kutoka Tanzania, ipo kama ifuatavyo.

Yanga SC imepangwa kucheza dhidi ya ASAS Djibouti Telecom ya Djibouti ambapo mshindi wa mechi hiyo atakutana na mshindi wa mechi kati ya AS Otoho ya Congo Brazzaville na Al Merrikh SC ya Sudan.

Simba SC itaanzia mechi za raundi ya pili (Second Round) ambapo itakutana na mshindi wa mechi ya African Stars ya Namibia na Power Dynamos ya Zambia.

KMKM ya Zanzibar yenyewe imepangwa kucheza dhidi ya St. George SC ya Ethiopia ambapo mshindi atakutana na mabingwa watetezi wa michuano hii Al Ahly SC ya Misri.

Mechi za raundi ya kwanza (First Round) zitachezwa kati ya Agosti 18 na 20 huku mechi za marudiano zikichezwa kati ya Agosti 25 na 27, Mechi za raundi ya pili (Second Round) zitachezwa kati ya Septemba 15-16 na marudiano kati ya 29-30.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *