Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Tanzania na Uganda watiana saini Ujenzi wa Bomba la Gesi

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Uganda zimetia saini mkataba mahsusi utakaowezesha kuanza kwa kazi ya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Gesi kutoka Tanzania kwenda Uganda.

Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Doto Biteko pamoja na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Jamhuri ya Uganda, Ruth Nankabirwa.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, kusainiwa kwa Mkataba huo kumetokana na Makubaliano ya Awali (Memorandum of Understanding – MoU) kati ya nchi hizi mbili yaliyosainiwa mwezi Agosti, mwaka 2018 kwa ajili ya ujenzi wa Bomba la kusafirisha Gesi Asilia kutoka Tanzania kwenda Uganda kutokana na Tanzania kugundua kiasi kikubwa cha gesi katika kina kirefu cha bahari na nchi kavu.

Ameongeza kuwa, Tanzania inaendelea kutafuta wabia wa kimkakati watakaoweza kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ili kutafiti na kuendeleza vyanzo vya upatikanaji wa mafuta na gesi.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini kutoka nchini Uganda Ruth Nankabirwa amesema kuwa, Uganda inatambua umuhimu wa mradi huu na kuongeza kuwa kumekuwepo na mahitaji makubwa ya matumizi ya gesi hivyo wana kila sababu ya kuhakikisha kunakuwepo na uharakishwaji wa mradi huo.

p

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *