Tanzania kuendelea kulinda haki za binadamu

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amesema Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika kulinda haki za binadamu kwa kuwa na sera nzuri zinazoongoza kulinda masuala ya jinsia.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Afrika wanaohusika na masuala ya Fedha na Jinsia kutoka nchi 22 Wanachama wa Jukwaa la Usawa wa Kijinsia.

Amesema katika kuhakikisha kuna usawa wa Kijinsia, Tanzania imeongeza idadi Wanawake kushika nafasi za uongozi katika maeneo mbalimbali, ikiwemo Serikalini.

Mkutano huo uliofunguliwa leo Novemba 15, 2023 na Rais wa Zamzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi utahitimishwa Novemba 17, 2023 ambapo wakati wa mkutano huo kutakuwa na mijadala na mada juu ya masuala ya fedha na usawa wa Kijinsia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *