Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika kusimamia usawa wa kijinsia kuanzia ngazi ya chini hadi kitaifa.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Leo Novemba 15 2023 mkoani Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa masuala ya Kifedha na usawa wa Kijinsia, unaojumuisha Mataifa 22 ya Afrika.
Amesema katika kuhakikisha Usawa wa Kijinsia unaendelea kuwepo nchini, Serikali itaendelea kutoa fursa sawa za uongozi na upatikanaji wa elimu hasa kwa Wanawake katika ngazi zote.
“Katika kuhakikisha tunatoa kipaumbele cha Usawa na Kijinsia, Serikali imeendelea kutenga fedha kwenye bajeti kuu ili kusaidia harakati za masuala hayo na kuwezesha watu wetu kupata haki sawa katika maeneo mbalimbali”. Ameongeza Rais Mwinyi