Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeeleza kuwa imeshandaa Sera ya masuala ya Akili Bandia ambayo inatoa muongozo wa namna ya kusimamia teknolojia hiyo inayokuwa kwa kasi duniani.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga wakati akifungua mkutano wa kwanza wa kimataifa wa wataalamu wa Akili Bandia ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kushirikiana na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha.
“Kama Taifa tupo tayari katika kutumia teknolojia hii ya akili bandia katika masuala ya tehama ili kuhakikisha matumizi ya teknolojia zinazokuwa kwa kasi zinatumiwa ipasavyo” amesema . kipanga.
Kipanga amesema akili bandia haijaondoa uhalisia wa akili za binadamu hivyo hayataharibu mfumo wa elimu bali utazidi kuimarika zaidi, huku akisisitiza kuwa vyuo vikuu vinatayarisha vijana kwa ajili ya kushiriki katika kuleta maendeleo zaidi.