Ahukumiwa miezi 21 kwa kosa la mtoto wake

DejaTaylor (26), mama wa mwanafunzi wa darasa la kwanza mwenye miaka 6, ambaye alimpiga risasi mwalimu wake mwezi Januari, amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela.



Deja amehukumiwa pia kwa kosa la kutumia dawa za kulevya aina ya bangi huku akimiliki bunduki ambayo mtoto wake aliichukua na kwenda nayo shuleni na kumpiga risasi mwalimu wake, #AbbyZweener.

Mwalimu Abby, ambaye kwa sasa anaogopa kufanya kazi hiyo ya kuwa karibu na watoto amefungua kesi ya dola milioni 40 dhidi ya Newport News School District kwa madai ya kupuuza taarifa yake ambayo aliwahi kuitoa juu ya kuwa na wasi wasi na mtoto kwamba anaweza kuwa na bunduki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *