Shule zafungwa kutokana na joto kali Sudan

Serikali ya Sudan Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kwa muda usiojulikana kutokana na wimbi la joto kali ambalo linaweza kusababisha viwango ya joto kuongezeka hadi nyuzi.

Mamlaka ya afya na elimu kwenye taifa hilo pia imewataka wazazi kuwazuia watoto wao kucheza nje kwa muda mrefu, wakisema joto hilo linaweza kudumu kwa wiki mbili.

Aidha mamlaka hiyo pia imesema kuwa tayari kumeripotiwa vifo vinavyohusiana na joto kupita kiasi.

Kwa mujibu wa mamlaka, shule yoyote itakayopatikana imefunguliwa kuanzia jumatatu, usajili wake utaondolewa.

Wiki iliyopita, takriban watoto 15 waliripotiwa kufariki kutokana na homa ya uti wa mgongo na magonjwa mengine yanayohusiana na joto, kulingana na wizara ya afya.

Baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki ikiwemo Kenya nayo pia yameripoti ongezeko la viwango vya juu vya joto haswa nyakati za usiku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *