Serikali imetoa siku 14 kuondolewa kwa namba za Magari zilizoongezwa ukubwa (3D), kwenye Magari yote yasiyoruhusiwa kuwekwa, namba zenye vibao vyeusi na zinazotumia namba za chasis, taa na stika ambazo zimeongezwa kwa matakwa ya wamiliki au madereva

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Jumanne Sagini amesema namba hizo hazitengenezwi na Wakala aliyepata kibali kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na pia herufi hizo zina ugumu wa kusomeka katika umbali usiopungua Mita 100