Wananchi wa kijiji cha Kimotorok, Kitongoji cha Oltotoi Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wameishukuru Serikali kwa kuwajengea Zahanati yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 153.
Wakizungumza mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga kukagua ujenzi wa zahanati hiyo wamesema kujengwa kwa zahanati hiyo kutawaondolea adha ya kutembea umbali mrefu ambapo kabla ya kujengwa kwa zahanati walilazimika kwenda zaidi ya kilometa 15 kufuata huduma za afya.

Aidha, Sendiga akiwa mahala hapo amewaagiza TANESCO pamoja na RUWASA kuhakikisha Zahanati hiyo inaunganishwa na huduma zao kwa haraka.