Rais wa Klabu yetu na Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu Afrika (ACA), Eng. Hersi Said amepata tuzo kutoka World Football Summit (WFS), ya kuthamini mchango wake wa kuunganisha Vilabu vya Soka Afrika.
Tuzo hiyo imetolewa wakati wa mkutano wa WFS, uliofanyika Jijini Rabat, Nchini Morocco.


