MKURUGENZI TANESCO AFARIKI DUNIA KWA AJALI

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamohanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali ya gari katika Wilaya ya Bunda, mkoani Mara.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Evans Mtambi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amefafanua kuwa limetokea kati ya saa 6 hadi 7 usiku wa kuamkia leo.

Mashuhuda wanasema chanzo cha ajali hiyo ni dereva gari dogo aina Land Cruiser aliyetaka kumkwepa Dereva wa Baiskeli ndipo alipogongana na lori ambapo pia dereva wa gari la hilo la Mkurugenzi naye amefariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *