Samia: msiwe waoga kufikiri wala kutoa mapendekezo

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi katika sekta mbalimbali kujali na kuthamini maendeleo, akisema kuwa ni haki ya Watanzania kuiona nchi yao ikiendelea.

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 14, 2023 , wakati wa uapisho wa viongozi mbalimbali Ikulu, Dar es Salaam na kuwapa neno viongozi hao.

“Tunapotaka maendeleo, Tanzania inayoendelea ni lazima tukae tupange tufikiri, na mimi niwaombe msione woga kwenda kufikiri wala kuja na mapendekezo ambayo mnayaona yanaweza kuendesha Tanzania vizuri.

“Kazi yenu ni kuwaza na kutuletea, halafu vyombo mbalimbali vitakaa tuangalie, kwa kipindi hiki sisi ndio tuliopewa dhamana ya kuleta maendeleo ya Watanzania kwa hiyo wote tukafikiri, tupendekeze, tuamue na tutekeleze kwa ajili ya Watanzania,” amesema Rais Samia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *