Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Halmashauri zenye uhaba wa watumishi wa afya kupewa kipaumbele

Serikali inatarajia kufanya tathimini ili kuzibaini halmashauri zenye uhaba mkubwa wa sekta ya afya ili kuzipa kipaumbele katika ajira mpya za kada ya afya

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hayo leo Julai 14,2023 akiwa katika ziara yake yan kikazi wilayani Kishapu na kuwaagiza wakurugenzi wa wilaya kuhakikisha wanawawezesha fedha za kujikimu watumishi wapya waliowasili katika vituo vya kazi.

Awali akiwasilisha taarifa ya afya wilaya kwa waziri wa afya,mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Modest Mkude amesema kwamba wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa watumishi,magari ya kubebea wagonjwa na upungufu wa vyumba vya huduma ya mama na mtoto.

Aidha ameiomba serikali kusaidia kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya ulionzishwa kwa nguvu za wananchi ambapo wilaya hiyo ina maboma zaidi ya 50 mpaka sasa na kuishukuru serikali kwa kupeleka watumishi wapya wa afya 32 katika wilaya hiyo.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo ameiomba wizara ya afya kutatua changamoto zilizoainishwa ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na kupongeza mabadiliko makubwa katika huduma za afya hali iliyopunguza malalamiko ya wananchi.

Aidha amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya miradi ya afya na vifaa tiba ambapo kwa mwaka huu bajeti ya dawa kwa wilaya hiyo imeongezwa hadi kufikia milioni 765.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *