Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Jambo Group yakabidhi jezi Mwamva FDC Queens

Kampuni ya Jambo Food Products mapema leo imekabidhi jezi seti mbili zenye thamani ya shilingi 500,000/= kwa timu ya soka ya wanawake ya Mwamva FDC Queens ya mjini Kahama, itakayoshiriki katika ligi ya mabingwa wa mikoa jijini Mwanza.

Mwamva FDC Queens ni mabingwa wa mkoa wa Shinyanga ambapo Mkurugenzi wake Mwalimu Aisa Mariki amesema mchango huo wa jezi ni motisha kubwa katika mashindano hayo ya ligi ya mabingwa wa mikoa yatakayoanza kutimua vumbi Julai 16, 2023 katika viwanja vya Alliance School Jijini Mwanza.

Akikabidhi jezi hizo, Mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Food Products, Chrispin Kakwaya ambaye ni Mkuu wa Idara ya Michezo Jambo Media amesemaKampuni hiyo ilipokea ombi kutoka Chama cha Soka mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) kuunga mkono timu hiyo hivyo kutokana na utamaduni wa Kampuni hiyo kusaidia jamii inayowazunguka ndiyo maana wametoa jezi hizo ili timu hiyo ikazitumie kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *