Rema ataja ugonjwa unaomsumbua kwa muda mrefu

Mwimbaji wa ngoma ya ‘Calm Down’, Rema kutoka Nigeria ameweka wazi kwanini anavaa miwani, ambapo amebainisha ni kwa sababu ana matatizo ya macho kwa muda mrefu, na hawezi kuona vitu vya karibu.

Rema amesema hayo katika mahojiano aliyofanya na Capital Xtra kwenye tuzo za Tuzo za Brit 2024 huko London, Uingereza hivi karibuni.

Rema anakuwa msanii wa pili kwa mwaka huu kutoka Nigeria kuweka wazi kuwa na matatizo ya macho. Ambapo Tiwa Savage alisema pia kuwa na tatizo hilo ambalo limekuwa likimfanya ashindwe kusoma vitabu na sasa anavaa miwani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *