Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

RC Macha amewataka wafanyabiashara mkoani Shinyanga kufanya biashara zenye ustawi kwa jamii

Wafanyabiashara Mkoani Shinyanga wametakiwa kufanya biashara zinazozingatia ustawi wa jamii ikiwa ni pamoja na kufuata sheria na taratibu zinazoongoza nchi kwa kutokufanya udanganyifu ili kuweza kunufaika na kuhakikisha serikali inapata tozo zitakazosaidia kukamilisha mipango mbalimbali ya maendeleo.

Rai Hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha wakati akifungua kikao cha baraza la biashara kilichoketi leo julai 17, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga ambapo amewataka wajumbe wa baraza hilo kuunda kamati za wataalamu ambazo zitasimamia maamuzi yatokanayo na baraza hilo, na kujadili fursa za kustawisha biashara.

Akizungumza katika kikao hicho Afisa kutoka Benki ya Serikali ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Kanda Ziwa Andrew Kimbelwa amesema Benki hiyo imeendelea kufanya mapinduzi katika sekta ya kilimo kwa kuwezesha kilimo biashara kwa wakulima, kwani wametoa zaidi ya shilingi bilioni 73 kwa wakulima katika Mkoa wa Shinyanga kwa jili ya ufadhili wa mahitaji mbalimbali kwa wakulima.

Baraza la Biashara la Mkoa ni kikao cha kisheria ambacho hukaa mara mbili kwa mwaka katika mkoa husika, na pia ni chombo pekee ambacho huwakutanisha wadau mbalimbali kutoka katika sekta za umma na binafsi pamoja na wawakilishi wa wafanyabiashara, lengo ikiwa ni kujadiliana na kuainisha changamoto na fursa zilizopo katika sekta ya biashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *