Rapa Post Malone amekanusha kuwa anatumia dawa za kulevya baada ya maswali kuibuka kutokana na mabadiliko kwenye mtindo wake wa kufanya show na muonekano wake.
Ameweka chapisho kwenye ukurasa wake wa instagram akisema “Situmii dawa za kulevya, nimeulizwa na watu wengi kuhusu kupungua uzito wangu na show zangu, na enjoy sana kufanya show zangu na niko na afya njema zaidi, toka nimekuwa Baba nimeanza kuacha vitu kama Soda na nimeanza kula vizuri zaidi ili niwe karibu na mtoto wangu kwa muda mrefu zaidi, kinachofuata ni kuacha kutumia, niko studio natayarisha muziki mpya na ninafuraha kwenye maisha yangu”.
Post Malone ana mtoto wa kike na mchumba wake, ambaye hajawahi kumuweka wazi kwenye mitandao ya kijamii au vyombo vya Habari.