Serikali kuandaa filamu ya maisha ya viongozi

Serikali kupitia Bodi ya Filamu inaratibu mpango mahususi wa uandaaji wa filamu zinazohusu maisha ya viongozi na historia ya nchi ikiwemo maisha ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma Aprili 28, 2023 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa anajibu swali la Mhe. Mussa Omar Salim (Gando) lililoulizwa kwa niaba yake na Mhe. Kassim Hassan Haji (Mwanakwerekwe) aliyeuliza mkakati wa serikali Katika kuandaa Filamu zinazoelezea historia ya nchi.

“Kwa sasa Bodi ya Filamu kwa kushirikiana na wadau wa filamu inaratibu mpango wa kuandaa filamu itakayoelezea maisha ya Bibi Titi Mohamed, Chifu Kingalu na Mtemi Mirambo” amesema Mhe. Mwinjuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *