Rais  Xi na Kansela Scholz wakutana Beijing

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz  hii leo amekutana  na Rais Xi Jinping mjini Beijing katika siku yake ya mwisho ya ziara ya siku tatu na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo ushirikiano wa kiuchumi, kijiografia na kisiasa huku pia wakigusia vita vya Ukraine, ulinzi wa hali ya hewa na mahusiano ya kibiashara baina ya nchi hizo.

Kansela Scholz amesema ataendelea kumsisitiza Rais Xi ambaye ana uhusiano wa karibu na Rais wa Urusi,Vladmir Putin juu ya athari ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine kuwa vita hivyo sio tu vimeliathiri bara la Ulaya bali hata ulimwengu mzima.

Mataifa ya Magharibi yamekuwa yakiishutumu China kwamba inaipatia Urusi bidhaa ambazo zinatumika kwa madhumuni ya kiraia na kijeshi na hivyo kuipa Urusi nguvu ya kiuchumi ya kuendeleza uvamizi wake nchini Ukraine.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *