Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Juni 15,2025 amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Mwanza tayari kwa ziara ya kikazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo umati wa Wananchi walifurika katika Uwanja huo kumpokea na kumshukuru kwa kuwaletea Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Baada ya kutua Mkoani Mwanza, Rais Samia ameelekea Mkoani Simiyu ambapo ndipo anapoanzia ziara yake ya kikazi.





