Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Rais Samia akutana na Papa Francis,waridhika na uhusiano wa Tanzania na Vatican

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye ziara yake ya kitaifa Vatican amekutana na kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki duniani, baba Mtakatifu Francis ambaye ndiye amempa mwaliko wa ziara hiyo.



Dhumuni la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania Na Vatican, na itakumbukwa mwaka 2016 hayati dkt. John Pombe Magufuli, alimwalika kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki duniani, yaani baba Mtakatifu Francis kutembelea Tanzania hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya ziara hiyo haikuwezekana na badala yake kwa wakati huu, rais Samia amealikwa na kiongozi huyo kufanya ziara Vatican.



Katika mazungumzo yao ya faragha yaliyodumu kwa takribani dakika ishirini na tano, wameridhika na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican Na Tanzania; Mchango wa kanisa katoliki katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu hususan katika sekta ya elimu, afya na ustawi wa jamii pamoja na changamoto ambazo Tanzania inapitia kwa sasa.

Takwimu zinaonesha kwamba, kanisa Katoliki nchini Tanzania linamiliki na kuendesha shule za awali 240, shule za msingi 147, shule za sekondari 244, vyuo vya ufundi, vyuo vikuu 5; taasisi za elimu ya juu 5 na vituo vya vyuo vikuu 2 ambavyo viko chini ya chuo kikuu cha mtakatifu Agustino, SAUT.,ambapo vyuo vyote hivi vina jumla ya wanafunzi 31, 000 pamoja na taasisi za afya 473.

Imepita takribani miaka 12 tangu rais mstaafu jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea mjini Vatican na kukutana na baba mtakatifu Benedikto Xvi tarehe 19 Januari 2012. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *