Aliyekuwa mchezaji wa Yanga, na sasa ni mchezaji wa wa Pyramids, Fiston Mayele ameweka wazi kuumizwa kwa kile kinachoendelea juu yake ambacho ni kusemwa vibaya na baadhi ya mashabiki wa soka wa Yanga.
Mayele ameweka ujumbe kwenye Instastory yake na kusema leo jioni ataongea kila kitu. Hapo jana Mshambuliaji huyo aliandika ujumbe unasomeka “CHUKI YA NINI MIMI SIO MTANZANIA ,NILIKOSEA KUCHEZA TIMU YA TANZANIA”.