Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Rais Dr. Samia awataka viongozi kutambua wajibu wao

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan amewasihi viongozi kuwa wawajibikaji na kutambua dhamana walizo nazo kwa wananchi na taifa kwa ujumla kama njia pekee ya kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine aliyeongoza nchi kwa misingi hiyo.

Ameeleza hayo leo katika kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha hayati Edward Moringe Sokoine mkoani Arusha ambapo amesema kuwa ni jukumu la kila kiongozi kuhakikisha utulivu ndani ya jamii kwa kuimarisha ushirikiano kwa kusimamia na kutekeleza kwa wakati masuala ya serikali kama ilivyopangwa kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi.

Aidha kutokana na uwepo wa athari za mafuriko, rais Samia ametoa salamu za pole kwa wakazi wa mikoa ya Pwani, Morogoro na Arusha sambasamba na ajali ya gari iliyobeba wanafunzi na kupoteza maisha ya wanafunzi sita na kuahidi kuendelea na ufuatiliaji wa athari za mafuriko hayo na kushughulikia zaidi  mahitaji muhimu na ya haraka kwa mikoa  iliyohathirika.

Pamoja na hayo rais Samia amesema mara baada ya mvua hizi zinazoendelea kunyesha kumalizika serikali itafanya uchunguzi wa kina katika maeneo hayo ya mabonde ambayo kihistoria hujirudia kuwa na matukio ya majanga ya mafuriko kwa lengo la kuja na suluhisho la kupunguza athari zinazojitokeza kwa kikipindi hiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *