Putin:Tunafanya Jitihada Dunia Isiingie Vitani

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesisitiza kwamba nchi yake itafanya kila liwezekanalo ili dunia isitumbukie kwenye vita lakini amesema kuwa Urusi haitakubali vitisho kutoka upande wowote.

Kauli hiyo ameitoa katika hotuba yake ya kuadhimisha Siku ya Ushindi wa umoja wa kisovieti dhidi ya manazi wa Ujerumani katika vita vikuu vya pili.

Amesema Urusi itafanya kila linalowezekana kuzuia mzozo wa kimataifa lakini wakati huohuo haitaruhusu mtu yeyote kuitisha na kudokeza kwamba Nguvu zao za kimkakati ziko tayari kila wakati.

Viongozi watano wa nchi ambazo zamani zilikuwa kwenye umoja wa kisovieti ambazo ni Belarus, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Turkmenistan na viongozi wengine kutoka nje ya umoja huo kutoka iongozi wengine washirika wa Urusi waliohudhuria ni kutoka Cuba, Laos na Guinea-Bissau walihudhuria sherehe hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *