![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2024/05/MADIWANI-1024x576.webp)
Na Costantine James,Geita
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mkoani Geita limelalamikia uwepo wa changamoto ya wanyama kama vile Viboko na Mamba ambao wamekuwa tishio kwa wananchi wanaoishi kandokando ya Ziwa Victoria na kuwafanya kuishi wakiwa na hofu ya kupatwa na madhara kutoka kwa wanyama hao hali inayosababisha shughuli za uvuvi na kilimo kukwama.
Hayo yamebainishwa leo (Mei 10,2024) na baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo wanaotoka katika kata kata ambazo zimezungukwa na ziwa Victoria wakati wa kikao cha kuwasilisha taaarifa mbalimbali utekelezaji wa shughuli za maendeleo ambapo wamesema mamba na viboko wamekuwa kuwa tishio kwa wananchi na kuiomba serikali kupitia idara ya maliasili kuchukua hatua za haraka kuwadhibiti wanyama hao.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt. Alphonce Bagambabyaki amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo katika baadhi ya maeneo ya halamashauri hiyo na kueleza kwamba sababu kubwa za uwepo wa mamba na viboko hao ni ongezeka la wanyama katika kisiwa cha hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo na kueleza kwamba wameanza kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na wanyama hao.
Afisa Maliasili Halmashauri ya wilaya ya Geita Asaph Manya amesema ili kukabiliana na changamoto hiyo kwa haraka zaidi pale ambapo tukio hilo linatokea Afisa Mtendaji wa kijiji husika anapaswa kuandika barua kwenda Mkurugenzi kuomba kibali ili wananchi waweze kuwasaka na kuwauwa wanyama hao ili kuondokana na hatari zinazoweza kusababishwa na wanyama hao kwa wananchi.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2024/05/AFISA-1024x576.webp)
Akifunga kikao cha Baraza la madiwani cha robo ya tatu kilichoketi mahsusi kwaajili ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za serikali kuanzia mwezi Januari hadi machi 2024, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Charles Kazungu amewataka watendaji mbalimbali wa serikali kutimiza majukumu yako Kikamilifu kikamilifu ikiwemo ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2024/05/DIWANI-1024x576.webp)