Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Prof. Janabi “Tatizo la ugonjwa wa figo ni kubwa”

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali Ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi Amesema Kuwa Tatizo La Ugonjwa Wa Figo Nii Kubwa Nchini Na Kwamba Matibabu Yake Yanahitaji Gharama Kubwa.

Prof. Janabi Ameyasema Hayo Jijini Dar Es Salaam Wakati Akizungumza Kuhusu Mbio Za ‘Figo Marathon’ Ziliandaliwa Na MNH Kwa Kushirikiana Na Klabu Ya Soka Ya Simba Na Taasisi Isiyo Ya Kiserikali Ya Heathier Kidney Foundation.

Amesema Ipo Haja Ya Jamii Kuunganisha Nguvu Katika Kuiunga Mkono Serikali Katika Matibabu Ya Magonjwa Ya Figo Kwa Kuwa Matibabu Yake Yanahitaji Gharama Kubwa.

“Tatizo La Ugonjwa Wa Figo Ni Kubwa Ambapo MNH (Upanga Na Mloganzila) Inahudumia Wagonjwa Wanaohitaji Huduma Za Kuchuja Damu Kwa Wagonjwa 130 Hadi 150 Kwa Siku Na Kusisistiza Kuwa Suluhisho La Kudumu La Matibabu Ya Figo Ni Upandikizaji,” Amesema

Naye Daktari Bingwa Wa Magonjwa Ya Figo, Dkt. Jonathan Ameongeza Kuwa Hospitali Inaendelea Kutoa Elimu Kwa Jamii Namna Ya Kukabiliana Na Magonjwa Yasiyo Ya Kuambukiza Ikiwa Ni Pamoja Na Kubali Mtindo Wa Maisha Kwa Kula Vyakula Kulingana Na Ushauri Kutoka Kwa Wataalam Wa Lishe Na Kufanya Mazoezi Na Kuepuka Tabia Za Kukaa Bwete.

Awali Akizungumza Mbio Za Figo Zinazotarajiwa Kufanyika Julai 9, Mwaka Huu Katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja, Dar Es Salaam, Msemaji Wa Klabu Ya Simba, Ahmed Ally Amesema Kuwa Klabu Hiyo Imekuwa Ikishiriki Katika Shughuli Mbalimbali Za Kijamii.

Mbio Hizo Zinalenga Kukusanya Fedha Kwa Ajili Ya Kusaidia Wagonjwa Wenye Matatizo Ya Figo Na Kuwasihi Washabiki, Wanachama Wa Simba Na Wananchi Kwa Ujumla Kushiriki Katika Mbio Hizo Ambazo Zinalenga Kuisaidia Jamii.

“Wapo Wananchi Wengi Wanakabiliwa Na Matatizo Ya Figo Wakiwemo Washabiki Na Wanachama Wa Simba Hivyo Ni Wajibu Wetu Sote Kujitokeza Kwa Wingi Katika Kuunga Mkono Mbio Hizi Ambazo Zinalenga Kuwasaidia Watanzania Wenzetu” Amesema Ally

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *