Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

China kununua bidhaa za kilimo Tanzania

Waziri Wa Viwanda na biashara Ashatu Kijaji Amekaribisha Uwekezaji Wa Kuzalisha Mafuta Na Bidhaa Nyingine Kwa Kutumia Matunda Ya Parachichi Ili Kuongeza Thamani Ya Zao Hilo Na Kuzalisha Ajira Kwa Wananchi.

Rai Hiyo Ameitoa Leo Jijini Changsha Alipokutana Na Mwenyekiti Wa Kampuni Ya Shanghai Grenchain Bi Rossella Lyu.

Kampuni Hiyo Ni Miongoni Mwa Makampuni Yanayonunua Parachichi Na Pilipili Kutoka Nchi Mbalimbali Ulimwenguni Kwa Ajili Ya Soko La China.

Kwa Upande Wake Bi Lyu Ameeleza Kwamba Kampuni Yao Ipo Tayari Kuanza Kununua Bidhaa Za Kilimo Kutoka Tanzania Sambamba Na Kuwekeza Katika Ujenzi Wa Miundombinu Ya Kuhifadhia Bidhaa Za Vyakula (Cold Storage Facilities).

Aidha, Bi LYU Ameahidi Kufanyia Kazi Mwito Wa Mhe. Kijaji Wa Kuwekeza Katika Uongezaji Thamani Wa Mazao Ya Kilimo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *