
Polisi wamefanikiwa kukamata tani 1.8 za madawa ya kulevya aina ya Cocaine kutoka katika mashua iliyokuwa imetia nanga kwenye bandari ya Marigot huko kisiwani Saint Martin kilicho chini ya utawala wa Ufaransa.
Vyanzo vinaeleza kuwa wahusika katika chombo hicho ambacho kinaelezwa kuwa na injini yenye nguvu kubwa, ambayo inatumiwa sana na wasafirishaji wa magendo walitoroka kabla ya kutiwa nguvuni.
Waendesha mashtaka wa umma katika kisiwa cha hicho wametoa ridhaa ya uchunguzi huo kwa mamlaka ya Saint Martin, kaskazini ambayo inatawaliwa na Ufaransa.
Mwaka 2022, mamlaka ya Ufaransa zilikamata tani 27.7 za Cocaine, ikiwa ni ongezeko la asilimia tano kwa 2021 ingawa muongo uliopita umeshuhudia ongezeko mara tano zaidi, madawa mengi yakiwasilishwa na usafiri wa majini.