Otieno kufuatilia tukio la kikatili alilofanyiwa Kalamba

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa Dodoma mtaa wa National Housing Kata ya Makole, Kalamba Ramadhani amelalamika kuteswa na watu anao wadhania kuwa ni polisi baada ya kumkamata kinguvu na kumfanyia vitendo vya ukatili ikiwemo kupigwa mpaka kujeruhiwa katika maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma ACP Martin Otieno Alipoulizwa na Jambo FM kuhusu tukio hilo amesema kuwa hana taarifa za tukio hilo bali ameahidi kulifuatilia kwa taratibu za kipolisi ili kujua ukweli wake, na kuongeza kuwa inapotokea haki za raia zimekiukwa na kuthibitishwa kuwa askari walitenda vitendo hivyo huchukuliwa hatua za kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *