Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Bidhaa zenye thamani ya sh. mil. 172 zakamatwa zikichepushwa

Operesheni iliyofanywa na mamlaka ya dawa,vifaa tiba na vitendanishi (TMDA ) imekamata dawa kadhaa zikiwemo dawa zenye asili ya kulevya na zile za nusu kaputi zilizokutwa kwenye maduka ya dawa ambazo haziruhusiwi kuuzwa nje ya hospitali zenye thamani ya Sh172 milioni, huku Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Simiyu ikitajwa kuwa vinara wa uchepushaji wa dawa.

Mkurugenzi Mkuu, Adam Fimbo Ameyamesema hayo leo Jumatano, Desemba 20, 2023 wakati akitoa matokeo ya operesheni maalum ya kukamata dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya Serikali, bandia, duni, zisizo na usajili na dawa za kulevya.

Fimbo amesema Vifaa tiba vya Serikali vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya Sh11,297,500 milioni vilikamatwa katika vituo na maduka binafsi, ambapo Baadhi ya vifaa tiba hivyo ni pamoja ni IV Cannula G21, G20, G22, vifaa vya kupima Malaria na Virusi vya Ukimwi, Hemocue Glocose201, Microcuvettes na Hemocue Hb2021 ambavyo vilikamatwa Kanda ya Mashariki na Kanda ya Kati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *