Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Ofisi ya CAG yatoa mafunzo kwa waandishi wa habari Shinyanga

Waandishi wa Habari nchini wameshauriwa kuandika habari,makala na kufanya chambuzi mbalimbali kupitia ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa serikali na taasisi zake.


Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) Bw.Focus Mauki wakati akiwasilisha mada katika semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari wanachama wa Klabu ya Waandhishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika Juni 28,2023 katika Ukumbi wa hoteli ya Karena.


Awali akifungua mafunzo hayo,Msaidizi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (AAG) Anna Masanja amesema vyombo vya habari vina jukumu la kuandika habari zinazojikita katika kuelezea hatua zinazochukuliwa na serikali katika kutekeleza mapendekezo ya ripoti za Ofisi ya CAG ili kuendeleza uwajibikaji nchini.


Semina hiyo kwa waandishi wa habari Mkoani Shinyanga imehusisha mada mbalimbali zinazohusiana na Ofisi na Ripoti za ukaguzi wa Mdhibiti na mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), aina za ripoti za ukaguzi pamoja na sheria, taratibu na kanuni za uendeshaji wa ofisi hiyo na nafasi ya waandishi wa habari katika kuripoti taarifa za ukaguzi na udhibiti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *