Mkandarasi umeme wa jua atambulishwa rasmi Shinyanga

Mkandarasi kutoka Kampuni ya Sinohydro Corporation ya nchini China, ametambulishwa rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi wa umeme wa Jua wilayani Kishapu kwa awamu ya kwanza.

Meneja Mradi wa umeme wa Jua kutoka TANESCO Makao Makuu Dodoma Mhandisi Emmanuel Anderson, akizungumza wakati wa utambulisho wa Mkandarasi huyo, amesema mradi wa umeme wa Jua wilayani Kishapu ni wa Megawatts 150, na utakuwa ukitekelezwa kwa awamu awamu.

Amesema Mkandarasi huyo kutoka Kampuni ya Sinohydro Corporation ya Nchini China, atatekeleza ujenzi wa umeme huo wa Jua wilayani Kishapu kwa awamu ya kwanza Megawatts 50.

“Leo tumekuja hapa kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kumtambulisha Rasmi Mkandarasi ambaye atatekeleza ujenzi wa mradi wa umeme wa Jua awamu ya kwanza Megawatts 50, na Mkataba wake wa ujenzi utaisha Agosti mwakani (2024),”amesema Mhandisi Emmanuel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *