“Nileteeni majina ya Wakurugenzi ambao hawajalipa Watumishi”

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amemuagiza Naibu Waziri, Deogratius Ndejembi kufuatilia Wakurugenzi ambao bado hawajalipa fedha za kujikimu watumishi wapya ili aone hatua za kuchukua dhidi yao.

Watumishi hao ni wale walioajiriwa katika sekta za afya Julai mwaka huu.

Mchengerwa ametoa agizo hilo jijini Dodoma kwenye mkutano Mkuu wa Umoja wa Walimu wa Shule za Msingi nchini (TAPSHA).

“Natambua kuna halmashauri Wakurugenzi wake bado hawajalipa stahiki za Watumishi wa Ajira mpya na nikitoa deadline ni mwezi wa kumi kama mpaka sasa kuna ambaye hajalipa nileteeni majina ya wakurugenzi hao. Tunachotaka kila mmoja wetu afanyekazi kwa kwa amani.”

“Niwaombe watumishi hawa wa ajira mpya mchape kazi tangulizenk maslahi ya taifa letu mbele, msiruhusu hata kidogo kukiuka maadili ya taifa letu niwaombe sana maskahi yenu mimi nitayashughulikia.”

Mchengerwa amesisitiza kuwa: “Nimekwisha kusema na nina rudia tena nitawalinda, nitalinda maslahi yenu ya walimu kote nchi nzima, sitakubali kuona uonevu wa walimu na nitayasimamia maslahi yenu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *