Hadi kufikia Juni 30, 2023 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilikuwa imesajili jumla ya walipa kodi 4,696,999, sawa na asilimia 16 ya idadi ya nguvu kazi iliyopo nchini ambayo ni takribani watu milioni 33.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi(BLW), Ameir Abdallah Ameir, aliyetaka kujua ni asilimia ngapi ya wafanyabiashara hawajaingizwa katika mfumo rasmi wa kodi na Serikali inachukua hatua gani kuwafikia.
“Hadi Juni 30, 2023 Mamlaka ya Mapato Tanzania ilikuwa imesajili jumla ya walipa kodi 4,696,999, sawa na asilimia 16 ya idadi ya nguvu kazi iliyopo nchini ambayo ni takribani watu milioni 33.