Staa wa muziki Diamond Platnumz ameeleza kuwa ngoma yake ya SHU imejua kuwaziba watu midomo na kuwataja kuacha kufanya uchambuzi kila anapotoa kazi.
Diamond Platnumz ameandika kupitia Instastory yake “Hii shu imejua kunidhalilishia watu, jamani mnapoona natoa ngoma punguzeni uchambuzi, maana niwazapo hamuwezi fika na sijawa tu msanii kwa bahati mbaya ni Mwenyezi Mungu alinijaalia niwe hivyo, kuna anavyonionyesha ambavyo akili yako haiwezi kamwe viona”.
Katika mitandao wa Youtube Audio ya SHU inawasikilizaji laki 712, na Video inawatazamaji Milioni 7.2.