Mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji ya Mohbad akamatwa

Msemaji wa Jeshi laJeshi la polisi Mjini Lagos-Nigeria, Bwn SP Benjamin Hundeyin, amethibitisha Jeshi hilo kwa sasa linamshikiria mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji ya Mohbad, promota Sam Larry.

Taarifa hiyo ya SP Benjamin Hundeyin, imetolewa na yeye mwenyewe kwenye ukurasa wake wa mitandao wa X, kwa kuandika “Balogun Olamilekan Eletu almaarufu Sam Larry kwa sasa yuko chini ya ulinzi wetu, Kwa sasa anasaidia uchunguzi unaoendelea wa kifo cha Mohbad.”

Mohbad amefariki Septemba 12, huko Lagos na kifo chake kimezua maswali mengi ikiwemo Promota huyo kutajwa kuhusika na mauaji pia msanii Naira Marley anatajwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *