Watu 52 wamefariki dunia baada ya kutokea kwa bomu na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa leo Ijumaa, Septemba 29, 2023 katika Mkoa wa Kusini Magharibi wa Balochistan nchini Pakistan.
Mlipuko umetokea wakati watu wakiwa wamekusanyika kusherehekea kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W).
Serikali ya Pakistan kupitia Jeshi la Polisi imesema bomu hilo ni shambulio la kujitoa mhanga lililolenga mkusanyiko huo wa kidini na tayari maofisa wametangaza hali ya hatari huku majeruhi wakipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
