Polisi Mkoani Morogoro wanafanya uchunguzi wa tukio la kukamatwa kwa mtoto Jonathan Yohana Sebastian (10), ambaye ni Mwanafunzi Darasa la tano aliyekuwa akiendesha gari aina ya Spacio yenye namba za usajili T 807 BVV mali ya Mwl. Zuhura Khatibu (47).
Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani humo iliyotolewa hii leo Mei 27, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa Alex Mkama, imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Mei 26, 2025 majira ya asubuhi huko eneo la Kigurunyembe, Wilaya ya Morogoro.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mtoto huyo akiwa na wenzake wanaotafutwa walitumia funguo bandia kufungua na kuendesha gari hilo na kwamba taarifa kamili itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.