SERIKALI MKOANI SINGIDA KUWEKA KIPAUMBELE KWENYE VYAMA VYA USHIRIKA

Na Saulo Stephen – Singida.

Serikali ya Mkoa wa Singida, imesema kuna umuhimu mkubwa wa kuweka vipaumbele vya kuanzisha na kuimarisha ushirika katika sekta za kilimo, ufugaji na madini ili kukuza kipato na uchumi mkoani Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ameyasema hayo wakati akizungumza na Umoja wa Vyama vya Ushirika Mkoani Singida na kudai kuwa kupitia ushirika umewezesha Wananchi kukua kichumi.

Amewasisistiza wanaushirika mkoani humo kuendelea kushirikiana katika vyama vyao kwani Serikali ya mkoa wa Singida ipo tayari kutoa ushirikiano watakaouhitaji lengo ni kufanya mkoa huo kukua zaidi kiuchumi kupitia vyama vya ushirika.

Kwa upande wake Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Singida, Nuria Gulamali amesema ili ushirika uweze kukua ni muhimu vyama viepuke kuwa vyama sisinzia vinavyoweza kupeleke kufutwa kwa vyama hivyo na kurudisha nyuma maendeleo na kuongeza kuwa ofisi ya mrajisi mkoani humo ipo wazi muda wote kwa ajili ya kushughulikia mambo mbalimbali yanayohusu vyama vya ushirika katika mkoa huo.

Naye mmoja wa wanaushirika, Joseph Dachi akizungumza na Jambo Fm mara baada ya jukwaa hilo amesema vyama vya ushirika vinapaswa kuwa na umoja ili kuhakikisha wanashirikiana ili kufikia malengo na kuiga mfano wa vyama vingine ambavyo vimekuwa vikishirikiana katika kutimiza malengo waliiyojiwekea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *