MLINDA MLANGO AFUNGIWA KWA UPANGAJI MATOKEO

Mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars na Klabu ya Kakamega Homeboyz, Patrick Matasi amesimamishwa kushiriki mashindano yote yaliyoidhinishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Kenya (FKF) kwa siku 90.

Mapema hii leo Machi 27, 2025, FKF iliarifu kufuatilia ukweli wa picha mjongeo, ambayo haikufahamika mara moja ni ya lini, ikimuonesha Mlinda mlango na watu wasiojulikana wakipanga kuhujumu matokeo ya mechi kadhaa za soka.

Kipa huyo, amekuwa akituhumiwa kufungwa magoli rahisi wakati akiichezea Timu ya Taifa na Klabu yake, huku FKF ikisema itachukua hatua kwa mujibu wa sheria za FIFA na CAF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *