WANAWAKE JITOKEZENI KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI – MNDEME.

Wanawake wametakiwa kujitokeza, kuchukua fomu na kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya udiwani,ubunge na kumuunga mkono
kiongozi mwanamke Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Christina Mndeme
ameyasema hayo wakati akiongea na Jambo FM katika msimu wa pili wa Chanuo
mada kuu ikiwani Ubunifu na Uongozi.

Mh. Mdeme amesema katika kipindi hiki cha Chanuo wanawake wachanue katika kuthubutu na kusimama katika uchaguzi na kuacha kusikiliza maneno ya kukatisha tamaa kutoka kwa baadhi ya watu ambao mara zote hawaamini nafasi ya mwanamke
katika kuongoza.


“Wanawake sisi tunaweza nimekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Tanzania bara, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa na sasa ni
Naibu Katibu Mkuu ninaweza, kwa hiyo mwanamke usiogope tunaye kinara mama
Samia na anatuongoza vyema” – Mndeme.


Akielezea dhana ya mwanamke kuonekana hawezi amesema katika safari yake ya
uongozi mara zote amekuwa akimtegemea na kumuheshimu Mungu na zaidi
ameendelea kumuomba ili ampe busara na hekima ya kujishusha na kumthamini
aliye juu na chini yake kwa kwa kufanya hivyo kila kitu kinawezekana.


Mndeme ameongeza kuwa mara zote amekuwa akitumia mbinu ya uvumilivu na
ushirikishaji pindi anapokutana na changamoto za kiuongozi.
“Uvumilivu imekuwa ni ngao yangu kubwa sana hasa ninapokutana na
changamoto za kiuongozi inapotokea natafakari kisha nafanya ushirikishaji
baadaye nakuja na solution si kila jambo unaweza kulitatua mwenyewe kwa hiyo
unapokutana na chagamoto kama kiongozi chukua akili yako changanya naya
mwenzio unapata suluhu” – Mndeme.


Aidha Mh. Mndeme ametoa wito kwa wanawake wote viongozi kuheshimu waume zao ambao ni baba wa familia na wasilinganishe nafasi zao za uongozi na kudharau waume zao.
“Mimi ni mama kiongozi ninapomaliza majukumu yangu Kitaifa nikirudi
nyumbani navua koti la uboss navaa koti la umama chini ya familia yangu na
majukumu yangu kama mama hayabadiliki hivyo mama kiongozi usijisahau
balance majukumu yako tambua familia na Taifa vyote vinakutegemea.” – Mndeme.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *