Timu za Michezo za Wanafunzi wa Shule za Msingi kutoka Halmashauri zote Mkoa wa Manyara, zimepiga kambi katika Shule ya Sekondari Singe iliyopo Halmashauri ya Mji Babati, kwa ajili ya kuunda timu ya Mkoa.
Afisa Michezo Mkoa wa Manyara, Samwel Pastory ameeleza kuwa kambi hiyo maalum ni ya muda wa siku tatu ikiwa ni maandalizi ya kuelekea mashindano ya Kitaifa yatakayoanza Juni 7, 2025 katika Mkoa wa Iringa.

“Jumla ya watoto 120 watawakilisha Mkoa wa Manyara kwa michezo ya Mpira wa Pete, Mpira wa miguu, Mpira wa kikapu, Riadha pia watoto wenye mahitaji maalumu watashiriki katika michezo hiyo,” ameeleza.


