MAENEO YA TAASISI YAPIMWE KUEPUKA MIGOGORO – DC NGATUMBURA

Na Saada Almasi – Simiyu. 

Mkuu wa wilaya ya Meatu, Fauzia Ngatumbura ameagiza mamlaka ya mipango Miji Wilayani humo kufuatilia suala la upimaji wa ardhi katika maeneo ya Taasisi, ili kuepuka migogoro ya ardhi siku za usoni.

Ngatumbura ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani wilayani humo na kusisitiza kwamba baadhi ya hayo maeneo yalitolewa na wazee hapo zamani hivyo kuzembea katika upimaji mapema kutazaa changamoto ambazo zitaleta kesi nyingi.

” sasa hivi hali itazidi kuwa mbaya maana maeneo mengi wazee wetu walipisha ili zijengwe zahanati,shule na vinginevyo sasa tuwe tunayaangalia haya mambo kwani msipofanya hatua ya ziadi hasa kwa maeneo ambayo tayari kesi zimeshaanza mjue kwamba tutatengeneza migogoro mingi ya ardhi” amesema Fauzia.

Sambamba na hilo Fauzia amesisitiza madiwani hao kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi juu ya uchangiaji wa chakula cha wanafunzi kwani hiki ni kipindi cha mavuno.

” zipo shule ambazo wanalima wao wenyewe kwa hiyo chakula siyo shida lakini wengine wasisitizeni kuendelea kuchangia chakula kwani wamelima,wamevuna chakula kipo kwa hiyo tusiwasahau hawa watoto wetu”

Utaratibu wa uchangiaji wa chakula kwa wanafunzi wanafunzi wawapo shuleni ni uchangiaji wa kawaida ambao unamhusisha kila mzazi kutoa kiasi cha fedha au chakula kitakqchomfanya mtoto kupewa mlo wa asubuhi na mchana kwa lengo la kuboresha ufaulu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *