Miaka 8 jela kwa kumuua mchepuko wa mume wake

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imemhukumu kifungo cha miaka 8 jela mkazi wa Kasamwa Wilaya ya Geita, Sumaye Mashaka (34) kwa kosa la kumuua bila kukusudia kimada wa mume wake, Asha Simba (34).

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Lilian Itemba baada ya mshtakiwa kukiri kosa bila kulazimishwa ambapo alimmwagia mafuta ya petroli kisha kuwasha kibiriti na kumuunguza sehemu mbalimbali za mwili wake na kupelekea kifo chake.

Akisoma maelezo ya awali, Wakili wa Serikali, Godfrey Odupy amedai mshtakiwa alikuwa akimtuhumu mume wake, Kisa Clement kwa kuingiza ndani ya nyumba yake vimada, na ilipofika Septemba 25, 2022 majira ya usiku, mshtakiwa alimfumania mume wake ndani ya nyumba yao akiwa na kimada huyo.

Ameongeza kuwa baada ya kitendo hicho mshtakiwa alimuunguza kimada huyo na kutokomea kusikojulikana, na Asha alichukuliwa na wasamaria wema hadi kituo cha polisi kwa ajili ya PF3 kisha akapelekwa hospitalini kutibiwa ambapo alifariki Oktoba 08, 2022 akiwa hospitali ya Rufaa ya Bugando.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *