MCHEZA MIELEKA MAARUFU REY MYSTERIO SR AFARIKI DUNIA.

Mcheza mieleka mstaafu wa (WWE), Rey Misterio Senior ambaye pia ni mjomba wa mcheza mieleka Rey Mysterio Junior, amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Jumamosi 21/12/2024 akiwa na umri wa miaka miaka 66.

Kifo cha Rey Misterio Sr. ni pigo kubwa kwa familia yake, sababu ni muda mfupi  baada ya msiba mwingine wa familia kutokea. Maelezo ya msiba wa mwanzo hayajatangazwa sana kwa heshima ya faragha ya familia. 

Familia imesema kupoteza wapendwa mara mbili mfululizo kumeongeza uchungu na huzuni. Jamii ya wanamieleka imekusanyika karibu nao, ikitoa msaada na rambirambi wakati huu mgumu.

Kifo cha nyota huyo wa mieleka kimethibitishwa na promotion ya mieleka kutoka Mexico Lucha Libre ambao pia ni watu wa karibu na familia ya Mysterio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *