KISHAPU: HOJA ZA CAG ZIFANYIWE KAZI – DC MASINDI

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.  

Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Peter Masindi amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na ofisi ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) kwa kuyafanyia kazi ili kutoendelea kuwepo kwa hoja hizo kwa kuzifunga kwa mujibu wa kanuni taratibu.

Dc Masindi ameyasema hayo leo Juni 13, 2025 wakati akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha  kwenye baraza maalumu la madiwani lililoketi leo katika ukumbi wa halimashauri hiyo kwa lengo la kujadili taarifa ya utekelezaji wa  mapendekezo ya CAG kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel ,amesema kwamba hoja 33 ambazo zipo kwenye utekelezaji zitashughulikiwa kwa wakati na kufungwa.

“Katika Hoja hizi 33 ambazo zipo kwenye utekelezaji, tutajitahidi kila kiambata kipelekewe kwa wakati ili hoja hizo zipate kufungwa,na tunampongeza pia Rais Samia Suluhu Hassan,sababu zile hoja za kisera nyingi zimeshajibiwa ikiwamo kuajiri Watumishi,” amesema Johnson.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Francis Manyanda amewaagiza Wakuu wa Idara,kuwa kila mmoja aanze kutafuta viambata ili kujibu hoja hizo na zifungwe, na kwamba katika Baraza lijalo mara baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wasikute hoja hizo.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Ibrahimu Makana,ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kupata Hati Safi,huku akisisitiza hoja za miradi viporo waiwekee kipaumbele ili waikamilishe.

Makana pia ameipongeza Halmashauri hiyo kwa usimamizi mzuri wa fedha za umma,pamoja na ukusanyaji wa mapato na kwamba Kishapu ya mwaka  2020, siyo ya sasa ambapo imepiga hatua kubwa kimaendeleo, huku akisisitiza kasi ya ukusanyaji mapato iongezeke, na yakusanywe kwa uaminifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *